Swahili Offline
Ningependa kuona lugha yetu ya kiswahili inawekwa offline, hii ni kwasababu Microsoft translator ni app mhimu sana kwetu katika kujifunza lugha ngeni lakini kutokana na kudorora kwa teknolojia kwenye jamii ya Afrika mashariki hii ni pamoja na ukosefu wa internet ya uhakika kwa muda wote inatuwia vigumu sana kupata huduma kwani hatuwezi kutumia application hii bila internet. Itakuwa na baraka kubwa sana kwetu endapo mtatuwezesha kuiweka lugha yetu offline. Nipo tayari kushirikiana nanyi katika hili. Ahsante sana.
